Ajibu amkuna Pondamali

Ajibu amkuna Pondamali


IBRAHIM AJIBU.

UWEZO unaoendelea kuonyeshwa na mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu, umemkuna golikipa wa makipa wa timu hiyo, Juma Pondamali, ambaye amemtabiria makubwa nyota huyo.

Ajibu juzi aliifungia timu yake bao pekee kwenye mchezo dhidi ya Ndanda FC katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Pondamali aliliambia Nipashe kuwa Ajibu anaweza akafanya vizuri zaidi msimu huu na kuisaidia Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa, kutetea ubingwa wake msimu huu.

"Kila mechi anaendelea kuonyesha kiwango cha juu, kwa kushirikiana na wachezaji wengine, Ajibu anaweza akasaidia timu kutetea ubingwa wake," alisema Pondamali.

Alisema anaamini baada ya muda mchezaji huyo ataonyesha makali yake yaliyoifanya timu hiyo kumsajili msimu huu akitokea kwa mahasimu wao, Simba ambao nao wanadhaminiwa na SportPesa.

Bao alilolifunga juzi linamfanya Ajibu kufikisha mabao mawili mpaka sasa katika michezo minne aliyoichezea timu hiyo msimu huu ambao ni wa kwanza kwake kukipiga Yanga.

Ajibu alianza kuifungia timu hiyo katika mechi dhidi ya Njombe Mji ambayo Yanga ilishinda kwa bao 1-0.

Post a Comment

0 Comments