Alichosema Mbunge Peter Msigwa wa CHADEMA baada ya serikali kusema ipo tayari kumlipia Tundu Lissu gharama za matibabu

Alichosema Mbunge Peter Msigwa wa CHADEMA baada ya serikali kusema ipo tayari kumlipia Tundu Lissu gharama za matibabu


Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kutoa kauli yake baada ya serikali kusema ipo tayari kulipia gharama za matibabu ya Tundu Lissu popote duniani na kusema huo ni utani wa serikali ya awamu ya tano.


Mbunge Msigwa alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kusema kuwa serikali ipo tayari kulipia gharama za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu popote duniani baada ya kupata maombi kutoka kwa familia ya Tundu Lissu na kama ripoti ya madaktari itaonyesha kuna ulazima kiongozi huyo kupatiwa matibabu zaidi basi serikali itasimamia jambo hilo.


Kutokana na kauli hiyo Msigwa amedai huo ni utani wa serikali "Huu ni utani wa serikali ya awamu ya tano" alisema Peter Msigwa


Mbali na hilo Mbunge Peter Msigwa alisema kuwa wao wanatambua thamani na umuhimu wa Tundu Lissu na kusema kuwa wapo tayari kuuza vitu vyao mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anapata matibabu na kurejea nchini akiwa salama.

Post a Comment

0 Comments