Serikali yaamua kukusanya mabaki ya kale

Serikali yaamua kukusanya mabaki ya kale


Serikali imeanza kukusanya mabaki ya kumbukumbu za binadamu zana na wanyama wakale yaliyopo katika maeneo mbalimbali na kuyarudisha kwenye makumbusho ya kale ya Olduvai Gorge ili kumbukumbu hizo zisitoweke na kuwafanya Watanzania na wageni kuendelea kuziona ndani ya makumbusho hiyo inayotajwa kuwa kubwa kuliko makumbusho zote zinazohifadhi kumbukumbu za zama damu katika bara la Afrika.

Mhifadhi wa Mambo ya Kale kutoka Makumbusho ya Taifa Dar-Es-Salaam Dk Agnes Gidna anasema lengo la kuzihifadhi kumbukumbu hizo ni kuelezea chimbuko na maendeleo ya binadamu ambayo Tanzania imekuwa na historia kubwa hasa katika mabonde la Oldvai na Laitori mahali palipogundulika fuvu la binadamu wa kwanza Zinja Thropus na nyayo za binadamu waliyoishi kwa zaidi ya mika milioni tatu.

Mhifadhi Msaidizi wa mambo kale kutoka kituo cha Oldvai George Olgo Mauyai anasema lengo lingine kuwezesha wanafunzi kushuhudia mabaki ya viumbe na zana za kale za mawe wanavyo soma kwenye vitabu Kaimu Meneja mahusiano wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ilipo Makumbusho Joyce Mgaya anasema vioneshwa hivyo vimetafitiwa kwa muda mrefu .

Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Fredy Manongi anasema wakati dunia ikiazimisha siku ya utalii duniani serikali ya Tanzania kupitia mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekuwa mafaniko mengi ya kujifunia ikiwemo uhifadhi wa mambo kale.

Post a Comment

0 Comments