Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani, LeBron James amewapongeza wachezaji wa ligi ya soka ya NFL na kikapu NBA kwa kufanya mgomo dhidi ya Rais Donald Trump huku akimchana Rais huyo kuwa anatumia michezo kuwagawa Wamarekani.
LeBron James
James (32) amesema hataruhusu mtu yoyote kutumia michezo kuwagawanyisha kwani wachezaji wote bila kujali aina ya mchezo, rangi, kabila wanawakilisha nchi .
”Hatuwezi kutumia michezo kama kitu cha kutugawa ni kitu cha ajabu tunapoona watu wanajaribu kufanya hivyo naamini wachezaji wote wanajielewa, Kwani licha ya maumbile, ukubwa, uzani, rangi , kabila au dini watu hukutana na kufurahi pamoja, Inawaleta watu pamoja”.amesema Lebron James kwenye mahojiano yake na UNINTERRUPTED
Maoni hayo ya LeBron James yamekuja baada ya Rais Trump kutweet mara kwa mara kwenye mtandao wa Twitter akidai kuwa wachezaji wa ligi ya soka nchini humo (NFL) ambao walishindwa kusimama wakati wa wimbo wa taifa ukiimbwa walifaa kufukuzwa au kusimamishwa kwa muda.
Hata hivyo wiki iliyopita mchezaji wa kikapu kutoka klabu ya Golden State Warriors , Stephen Curry alikataa wito wa Rais Trump wa kuzuru White House, ambapo timu yake iliitwa na Rais Trump.
James anayekipiga kunako klabu ya Cleveland Cavaliers alikuwa upande wa Hillary Clinton ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Rais Trump kwenye uchaguzi mkuu wa urais nchini humo mwaka jana.
0 Comments