Mauzo ya’ Sugarcane’ yampagawaisha Tiwa Savage

Mauzo ya’ Sugarcane’ yampagawaisha Tiwa Savage


Mixtape ya ‘Sugarcane’ kutoka kwa mwanadada Tiwa Savage, imeanza kufanya vizuri sokoni ikiwa ni siku chache toka itinge sokoni.
Mixtape hiyo yenye ngoma sita imekuwa ikiuzwa kwa njia ya mitandao kama Apple Music na iTunes imeweza kushika namba moja kwa mauzo.
Kupitia mtandao wa Instagram mrembo huyo aliposti kushukuru mashabiki zake kwa kumsapoti na kuandiaka “Baba God, you too mush 🙏🏼🙏🏼🙏🏼 #SugarCaneEP #SMD #323ENT #ROCNATION#SavageSoldiers.”
Ukianchana na ngoma ya ‘Sugarcane’ inayobeba mixtape hiyo kuna ngoma kama ‘Ma Lo’ aliyomshirikisha Wizkid na Spellz, ‘Get It Now’, ‘Me & You’ na ‘Hold Me Down’ pia inapatikana kwa kiasi cha dola 5.94 sawa na kiasi cha shilingi 13,327.53 za kitanzania.

Post a Comment

0 Comments