Mr. T Touch atoa ya moyoni, ‘mwisho wa siku tutajua mbivu na mbichi’

Mr. T Touch atoa ya moyoni, ‘mwisho wa siku tutajua mbivu na mbichi’


Producer wa muziki Bongo, Mr. T Touch ameeleza ya moyoni kwa baadhi ya mambo ambayo anakabiliana nayo kwa sasa.
Mr. T Touch ambaye pia ni C.E.O  wa Touchez Sound ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kueleza hisia zake kuhusu mambo kadhaa ila hajaweka wazi ujumbe huo unamlenga nani moja kwa moja.
Huwa sishangai binadamu anapokuwa fake#bandia kwenye maisha yangu na akawaaminisha watu kwamba ana msaada kwangu hiyo haijawai kuniumiza coz toka zamani nimekuwa mtu ambaye nikijua marafiki wanafiki na nikaishinao najua kwamba hawataki kusema mbele za watu kwamba nina mchango kiasi gani kwenye maisha yao lakini nafsi zao zinajua nilipambana kiasi gani mwisho wa siku tutajua mbivu na mbichi hapa hapa duniani coz wamekuwa ni watu wa kuongelea hata vile ambavyo hawajawai kuvifanya kwenye maisha yangu yale wanayoyakusudia na yale niliyoyashuhudia na kuyaona kuhusiana na maisha yangu yanatosha kabisa kujiamini na kusonga mbele japo najua ipo siku isiyokuwa na jina watajua nini namaanisha.
Producer Mr. T Touch kwa mwaka huu ameweza kufanya kazi na wasanii wakubwa kama Jay Moe, Professor Jay, Young Dee, Dayna Nyange, Young Killer, Roma na Stamina (Rostam) na wengineo.

Post a Comment

0 Comments