Kwa hesabu za mamlaka ya viwanja vya ndege, kuna ongezeko la wasafiri kwa soko la ndani.
Matatizo ya Precision yamekuwapo kwa muda mrefu sana. Mara tu baada ya kuondoka CEO (Mkenya) aliyepita, walijikuta wakiwa na madeni makubwa sana yaliyosababishwa na maamuzi ya kibiashara yasiyo na tija. Maamuzi hayo ni pamoja na manunuzi kwa bei zisizo na uhalisia kama ukodishaji wa ndege, matengenezo ya ndege, huduma, na manunuzi ya bidhaa zinazohusiana na uendeshaji wa shirika la ndege.
Baada ya kujitengeneza madeni makubwa, walipatwa na balaa lingine la kupotea kwa umilki wa soko baada ya fastjet kuanza safari zake huku wakijificha nyuma ya bei za chini ili kumuangamiza precision kisha watoze bei kubwa. Precision mwenyewe kama sio huo ubabe wa fastjet angetumaliza kwa bei za juu ili kufidia madeni yake kwa kusaidiwa na ukiritimba (monopoly) wa soko aliokuwanao.
Hivyo pamoja na uhuni wa fastjet, kuna faida pia kuwa alituepusha watanzania na balaa la kufidia madeni ya precision yaliyotokana na uzembe wa menejimenti hasa CEO na mkuu wao wa fedha CFO (mkenya pia). Hicho kidogo walichokuwa wakiambulia baada ya ujio wa Fastjet kimezidi kupungua baada ya ATCL kuingia kazini.
Makali ya madeni yao sasa ni dhahiri na hawana jinsi bali kufunga mikanda na kuhakikisha hawafi au kufilisiwa kwa madeni. Kumbuka kuwa hadi sasa hawajamaliza kulipa mikopo ya ndege zao walizonunua kwa udhamini wa benki fulani na mashirika ya fedha ambayo huruma ya kukukopesha huisha ghafla unaposhindwa au kuonyesha kuwa uwezo wa kulipa umepungua.
Kenya airways anafuatilia kwa makini dalili za kifo cha precision maana ni faraja kwake. Nasema ni faraja maana alikuwa na uwezo wa kumnusuru toka zamani kama angetaka kufanya hivyo. Alikuwa na uwezo wa kumpa ndege kubwa precision kwa ajiri ya safari za masafa marefu kutoka Dar es salaam moja kwa moja lakini hakutaka kufanya hivyo ili amtumie kama ndoo ya kujaza pipa.
Kumruhusu Precision kuwa na uwezo huo kungepunguza abiria ambao wanapelekwa kujaza ndege za Kenya airways hapo Nairobi. Precision akikaribia kukata roho si ajabu Kenya airways akamsaidia asikate roho kwa kuweka fedha kwa masharti kuwa mtaji wa kenya airways ndani ya Precision utaongezeka na kumuacha kilema badala ya kufa kabisa. Kwa ufafanuzi huu wa hali ya chini ni wazi kuwa swala la kupunguza wafanyakazi wa precision halihusiani na Makali ya Uchumi wa Magufuli bali ubadhirifu wa uongozi uliopita, kufuka kwa ATCL na ushindani toka Fast Jet, na ujanja wa Kenya Airways.
0 Comments