Kikosi cha klabu ya Rayon Sports ya Rwanda kimewasili nchini tayari kuwakabili Yanga SC mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Mei 16 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga itashuka dimbani huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa awali uliopigwa jijini Algiers huko Algeria.
Rayon ambao wametua nchini wamefanikiwa kutoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya Gor Mahia FC katika mchezo wake wa kwanza uliopigwa Amahoro Stadium jijini Kigali Rwanda.
Kuelekea mchezo huo tayari viingilio vimeshatajwa ambapo VIP A itakuwa Tshs 15,000, VIP B na C ni 7000 na mzunguko itakuwa ni Tshs 3000 pekee.
0 Comments