Alisson Becker tayari ametua Anfield kwa ajili ya vipimo

Alisson Becker tayari ametua Anfield kwa ajili ya vipimo

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Brazil na zamani klabu ya AS Roma Alisson Becker tayari ametua katika viunga vya Anfield kwa ajili ya vipimo vya kiafya ili kuanza kuitumikia klabu hiyo.


Liverpool wamefikia makubaliano na klabu ya AS Roma ya Italia kwa ada ya uhamisho wa Euro mil 67 za kumnunua mlinda mlango huyo ambaye ni miogoni mwa walinda milango bora kwa sasa duniani.

Liverpool wamekuwa na tatizo la kupata walinda mlango ambao wamekuwa na wakati mgumu sana hasa linapokuja suala la kuisaidia timu katika michezo muhimu zaidi.

Alisson Becker aliisaidia AS Roma hadi kufika hatua ya nusu fainali katika michuano ya UEFA Champion League na katika mchezo wa mwisho wa nusu fainali Liverpool ndio timu ambayo iliiondosha AS Roma kwa tofauti kubwa ya magoli ambayo ilikuwa ni 7-6.


Mkurugezi wa AS Roma Monchi amethibitisha hilo akiongea na Sky in Italy kwa kusema “Wakati ofa kubwa inapokuja hunabudi, unapaswa kuzingatia. Tulipima faida na hasara na tukaamua ni bora kuzungumza na Liverpool”

Monchi aliongeza “kumuuza Alisson hakuonyeshi kuwa tulikuwa na ukosefu wa tamaa. Kwa mimi, tamaa ni juu ya kufanya jambo sahihi baada ya kufikiri kila kitu kupitia kitu hicho”


Alisson alicheza michezo 49 msimu uliopita ukijumuishwa mchezo wao dhidi ya Liverpol ambapo matokeo yalikuwa 7-6,lakini pia ndio anakuwa mlinda mlango ghali zaidi duniani baada ya mlinda mlango wa Manchester City Ederson kununuliwa Euro mil 47 akitokea Benifica.

Post a Comment

0 Comments