Jeshi la polisi mkoani Dodoma limewataka baadhi ya madereva Bodaboda na Bajaji kuacha tabia ya kushiriki katika uhalifu ikiwemo baadhi ya madereva hao kushiriki katika vitendo vya ubakaji kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na unyang'anyi wa kutumia silaha.
Akizungumza na madereva wa Bodaboda na Bajaji Jijini Dodoma kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto amesema mbali na kushiriki katika ubakaji lakini wapo wanaoshiriki katika vitendo vya unyang'anyi wa kutumia silaha.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa madereva Bodaboda jijini Dodoma Lucas Kung'aro amesema wapo baadhi ya madereva wachache ambao wamekuwa hawafuati sheria za usalama barabarani ambao wamekuwa wakisababisha ajali za barabarani na wengine kufanya vitendo vya uhalifu.
ITV imezungumza na baadhi ya madereva wa bodaboda ambapo wameziomba mamlaka husika kuwachukulia hatua madereva ambao hawatii sheria za usalama barabarani na pia wanaoshiriki katika vitendo vya uhalifu
0 Comments