Maurizio Sarri ametangazwa rasmi kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea na kurithi mikoba ya Antonio Conte ndani ya Stamford Bridge.
Conte ametimuliwa hapo jana siku ya Ijumaa baada ya ufalme wake wa miaka miwili kwenye klabu hiyo iliyopo Magharibi mwa jiji la London.
Sarri ameachana na timu yake ya zamani ya Napoli na kutua Chelsea baada ya kuinoa kwa misimu mitatu klabu hiyo inayo shiriki ligi ya Serie A huku aliyekuwa meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti akitarajiwa kupokea kijiti cha kukinoa kikosi hicho.
Mara baada ya utambulisho huo Sarri amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kuwa ndani ya Klabu ya Chelsea na ninafasi nyingine katika taaluma yake ya ufundishaji.
Sarri anatarajia kusafiri siku ya Jumatatu hadi nchini Australia kwaajili ya kukutana na kikosi cha wachezaji wa Chelsea pamoja kujiunga na benchi zima la ufundi akiwemo mchezaji wa zamani wa timu hiyo Gianfranco Zola.
0 Comments