Mbunge wa Tarime Mjini , Esther Matiko (CHADEMA) amefunguka kuwa katika vitu vilivyowahi kumuumiza tangu aingie kwenye siasa ni pamoja na kuondoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbrod Slaa.
Matiko amefunguka hayo kupitia Kikaangoni ya EATV ambapo amesema kuwa amewahi kuumizwa na siasa pindi kiongozi huyo alipoondoka wakati chama kikimhitaji.
“Dkt. Wilbrod Slaa ni kiongozi aliyeniumiza sana wakati alipoondoka ndani ya chama kwa kuwa aliondoka kipindi ambacho kila mtu hakutegemea, ni kama mwanajeshi mko vitani kisha akaamua kuwageuka njiani”, amesema Matiko.
Aidha ameongeza kuwa, “Zitto ni kiongozi ambaye ana nafasi yake kwa vijana wa taifa hili. alipoondoka CHADEMA niliumia lakini nilimtakia kila la kheri kwa huko alipochagua kwenda”.
Septemba 1, 2015 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbrod Slaa, ambaye kwa sasa ni balozi wa Tanzania nchini Sweden, alitagaza rasmi kuondoka katika chama hicho na kustaafu mambo ya siasa.
0 Comments