Mimi kushiba nimeelekezwa juzi na dokta, kwamba ukishiba unajisikiaje – Peter Msechu

Mimi kushiba nimeelekezwa juzi na dokta, kwamba ukishiba unajisikiaje – Peter Msechu

Msanii wa muziki Peter Msechu amedai katika wakati wake wote wa maisha alikuwa hajui kushiba nini mpaka siku ya juzi alivyoelekwezwa na madaktari maana ya kushiba.

Muimbaji huyo amedai alikuwa anakula mpaka tumbo lake lijae au meno yake yachoke kutafuna ndipo anapoacha kula chakula.

“Wali maharage ni tatizo kubwa kwa vijana tupunguze jamani” Msechu alikiambia EFM. “Mimi nilikuwa sijui kushiba ni nini, nakula mpaka meno yachoke kutafuna au tumbo lijae, sana.”

“Kuna wakati nilifikia mpaka kilo 140 daktari akaniambia Msechu jiangalie, utapoteza maisha. Daktari ndio akaanza kuniambia maana ya kushiba nikaanza kuelewa kidogo lakini wali na maharage tukae nao mbali sana vijana,”

Msechu amedai kwa sasa ameweza kusikiliza ushauri wa daktari wake na tayari mwili wake umenza kubadilika.

Post a Comment

0 Comments