Timu ya taifa ya Ubelgiji imefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya Uingereza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya kombe la dunia.
Mchezo huo uliyopigwa kwenye dimba la Krestovsky Ubelgiji ilipata mabao yake kupitia kwa wachezaji wake, Thomas Meunier dakika ya nne na Eden Hazard dakika ya 82.
Mara baada ya mechi hiyo macho na maskio ya wapenzi wa soka wanayaelekeza hiyo kesho siku ya Jumapili kwenye mchezo wa fainali wa kombe la dunia baina ya Ufaransa dhidi ya Croatia.
0 Comments