Polisi Morogoro yaonya madereva wanaoleta ujanja ujanja

Polisi Morogoro yaonya madereva wanaoleta ujanja ujanja



Kufuatia operasheni za mara kwa mara zinazofanywa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa magari yaendayo mikoani zimeanza kuleta matokeo ambapo jumla ya leseni 4,734 zimekaguliwa na madereva tisa wamefikishwa mahakamani kati yao watano wamehukumiwa kifungio cha miezi minne jela na faini ya shilingi elfu kumi.

Akizungumza mara baada ya kugagua magari yaendayo mikoani katika kituo cha mabasi Msamvu Morogoro kamanda wa polisi mkoani hapa Wilbrod Mutafungwa amesema zoezi hilo la ukaguzi wa magari ni endelevu hivyo wamewafikisha mahakamani Madereva Tisa ambao kati yao watano wamehukumiwa kifungo cha miezi minne jela na faini ya shilingi elfu kumi ili iwe fundisho kwa madereva wengine

Pia kamanda Mutafungwa amewataadharisha abiria ambao wanatabia ya kumshawishi na kushabikia dereva kuendesha kwa mwendokasi kuacha tabia hiyo kwani zoezi hilo ni muhimu sana kwa ni linaokoa maisha yao

Kwa upande wa mmoja wa madereva wa mabasi Hashim Mohamedi Jamila Peter wamelishukuru jeshi la polisi wameshauri zoezi hilo liwe enderevu pia litolewe kwa madereva wote pia suala la muda lilikizingatiwa

Post a Comment

0 Comments