TFF wafanya mabadiliko kwa wacheji ligi kuu

TFF wafanya mabadiliko kwa wacheji ligi kuu

KLABU za Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuanzia msimu ujao zitaruhusiwa kutumia wachezaji wote 10 wa kigeni zitakazowasajili kuanzia msimu ujao wa 2018-2019.

Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kilichofanyika Julai 12, mwaka huu Makao Makuu ya TFF Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.

Pamoja na Kamati ya Utendaji ya TFF chini ya Rais wake, Wallace Karia kupitisha kanuni mbalimbali ikiwemo kupitisha usajili wa idadi ya wachezaji 10 wa kigeni katika Ligi Kuu kuanzia msimu ujao, pia imeridhia wote wacheze kwa wakati mmoja.

“Wachezaji hao wa kigeni wanaweza kutumika wote kwa wakati mmoja kulingana na mahitaji ya klabu. Uamuzi huo umelenga katika kuboresha na kuleta ushindani zaidi kwenye Ligi pamoja na kupandisha viwango vya wachezaji wazawa,”imesema taarifa ya TFF.

Katika hatua nyingine kikao hicho cha kamati ya Utendaji kimemuondoa Clement Sanga aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB) kwenye nafasi hiyo kwa kukosa sifa baada ya klabu ya Yanga kuwasilisha barua iliyokuwa na maelezo ya kwamba Yusuph Manji ndio mwenyekiti wa klabu hiyo.

Kamati ya Uchaguzi imeelekezwa kuandaa uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo kamati ya utendaji imekubaliana kamati ya uchaguzi kuelezea mchakato mzima wa uchaguzi ulivyokuwa wakati Sanga anaingia Bodi ya Ligi.

Post a Comment

0 Comments