Jeshi la Polisi nchini limetoa onyo kali kwa watu wanaofanya vitendo vya uhalifu katika bahari, maziwa na mito mikubwa hapa nchini kuacha mara moja kwa kuwa wamejipanga kuhakikisha wavuvi wanakuwa salama wakati wanapofanya shughuli zao.
Kauli hiyo imetolewa na IGP Simon Sirro Jijini Mwanza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya askari polisi wanamaji yaliyokuwa yakifanyika katika Chuo cha Polisi Wanamaji kilichopo Jijini humo.
Aidha IGP Sirro amewataka wazazi kuwakanya watoto wao kutojihusisha na vitendo vya uhalifu kwa kuwa serikali ya awamu ya tano haina mchezo na wahalifu.
IGP Sirro yupo ziarani katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa kukagua utendaji kazi wa Polisi na kuzungumza na wananchi waishio katika visiwa ili kuimarisha usalama hususani kwa wavuvi
0 Comments