Beyonce afunguka kuhusu upasuaji aliofanyiwa

Beyonce afunguka kuhusu upasuaji aliofanyiwa



Ifahamu hii siri nyingine kutoka kwa staa Beyonce ambaye amefunguka na kusema kuwa alifanyiwa upasuaji kipindi cha kujifungua watoto wake mapacha Rumi na Sir na amelithibitisha hilo katika jarida la Vogue hii ni baada ya kuzungumzia muonekano wake kipindi baada ya kujifungua.

Beyonce amefunguka na kusema kuwa kipindi cha ujauzito wa watoto wake mapacha aliongezeka uzito na kufikia hadi kilo 98 hali ambayo ilimfanya ashindwe kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na kuishiwa nguvu na hali hiyo ilionyesha kuhatarisha maisha ya watoto wake na hivyo ilibidi afanyiwe upasuaji unaofahamika kama (Cesarian Section).

“Nilikuwa na kilo 98 siku ambayo nilijifungua watoto wangu Rumi na Sir, na nilikuwa katika chumba cha mapumziko kwa mwezi mmoja kutokana na tatizo la toksemia, hali yangu pamoja na watoto haikuwa nzuri kwahiyo nilifanyiwa upasuaji wa haraka unaojulikana kama C-Section na tulikaa NICU kwa wiki kadhaa”


Beyonce alifunguka zaidi na kusema kuwa baada ya watoto hao kuzaliwa walibidi wawe chini ya uangalizi wa madaktari na hivyo walipelekwa chumba maalumu cha uangalizi na walikaa kwa wiki kadhaa, pia anamshukuru sana mume wake Jay Z kwa kuwa rafiki wa karibu na baba bora kutokana na kuonyesha ushirikiano katika kipindi hicho kigumu.

Post a Comment

0 Comments