Watu13 wafikishwa Mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi

Watu13 wafikishwa Mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo watu 13 wamefikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwemo utakatishaji fedha wa Shilingi Milioni 154.

Akiwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kelvin Mhina wakili wa serikali mkuu, Nassoro Katuga amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 5 ambayo wameyatenda katika mikoa tofauti.

Katika kosa la kwanza la kula njama ya kutenda kosa linawakabili washtakiwa wote ambapo wanadaiwa wamelitenda kati ya March 2018 na June 2018 katika jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Rukwa na katika maeneo mengine ya Jamhuri ya Tanzania.

Pia kosa jingine ni kusambaza taarifa za uongo kupitia mfumo wa kompyuta ambapo wanadaiwa wamelitenda March na June 2018 wakiwa Dar es Salaam na Rukwa ambapo walichapisha taarifa fupi za jumbe (Message) ili kujipatia kitu.

Wakili Katuga amedai kosa jingine ni kusambaza jumbe (message) kwa njia ya Elektroniki kati ya March na June, 2018 kwa nia ya kudanganya na kushawishi kati ya Dar es Salaam na Rukwa walisambaza kwenda kwa watu tofauti tofauti ili kuonyesha wana mamlaka hayo.

Pia katika kosa jingine la kusambaza jumbe fupi za Kielektroniki, wanadaiwa walilitenda March na June, 2018 kati ya Dar es Salaam na Rukwa walisambaza jumbe zisizotakiwa kwa njia ya Kielektroniki.

Katika kosa la mwisho wanadaiwa ni utakatishaji fedha ambapo wanadaiwa wamelitenda kati ya March na June 2018 katika maeneo ya Dar es Salaam na Rukwa.

Inadaiwa kwa pamoja walijihusisha katika ufanyaji wa muamala wa Sh.Mil 154,032,830 ikiwa ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Katuga amedai upelelezi haujakamilika ambapo Hakimu Mhina amesema kesi hiyo haina dhamana kwa sababu ni ya uhujumu uchumi, hivyo wataenda lumande ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi August 21,2018.

Katika kesi hiyo washtakiwa Boniface Maombe, David Luvanda, Moshi Sungura, Amos Bosco, Lule Kadenge, Jofrey Kapangamwaka, William Nturo, Regius Mauka, Collins Basham, Francis Kapalata, Kasonde Kapela, Enock Mwandaji na Pascal Kiatu.

Post a Comment

0 Comments