Rais John Magufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa 34 wa Jumuiya ya Serikali ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat). Mkutano huo utafanyika Septemba 24 hadi 28 mwaka huu na kushirikisha wajumbe 500 wakiwemo wataalam na wageni waalikwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat) ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Gulam Hafeez Mukadam amesema hayo mjini Dodoma.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni Umuhimu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa Huduma na Ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa viwanda.
Amesema mkutano huo unalenga kubainisha mamlaka za serikali za mitaa zipo karibu zaidi na wananchi na zinatoa huduma na kubainisha umuhimu wa wananchi katika kubuni na kusimamia miradi ya maendeleo na kuibua fursa za uwekezaji viwanda kufikia uchumi wa kati.
Amesema agenda zitakazojadiliwa pamoja na mambo mengine kujadili taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa shughuli za jumuiya, taarifa za fedha na kupitisha bajeti ya mwaka 2018/2019.
Makamu Mwenyekiti wa Alat na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa, Steven Mhapa aliitaka Alat Mkoa kufanya mikutano yao mwishoni mwa mwezi huu na taarifa za vikao hivyo kupelekwa kwa Katibu wa Alat ili zijumuishwe kwenye taarifa ya Jumuiya.
Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe alisema mkutano huo utakuwa na usalama akitaka wananchi kutumia fursa hiyo. Mukadam alisema michango ya wanachama haikuwa vizuri kwa sasa uongozi wake umejipanga kuhakikisha wanachama wake wanalipa madeni.
" Tumepanga kuweka mazingira ya kuhakikisha wanachama wanatoa michango na hii si kwa ajili ya mkutano huo pekee bali kuhakikisha wanajenga jengo la kitega uchumi jijini Dodoma kwa ajili ya wana Alat," amesema na kuongeza mkutano huo utagharimu sh milioni 300
0 Comments