IGP Sirro alizwa na msiba wa Wafanyakazi wa Azam Tv, Aagiza uchunguzi ufanyike upesi kubaini chanzo cha ajali

IGP Sirro alizwa na msiba wa Wafanyakazi wa Azam Tv, Aagiza uchunguzi ufanyike upesi kubaini chanzo cha ajali


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro ameagiza kufanyike uchunguzi wa chanzo cha ajali ya magari mawili iliyotekea mapema leo Julai 8, 2019 asubuhi katika kijiji cha Shelui mkoani Singida na kusababisha vifo vya watu 7 wakiwemo wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media.


IGP Sirro
IGP Sirro ametoa agizo hilo leo Julai 8, 2019 akiwa jijini Mwanza katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za polisi eneo la Myamhongolo, Kwa kutaka uongozi wa jeshi la polisi mkoani Singida kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote atakayebainika kuwa chanzo cha ajali .

Wafanyakazi hao wa Azam TV na abiria wengine walikuwa wanaenda kwenye hafla ya Uzinduzi wa Hifadhi ya Burigi-Chato unaotarajiwa kufanywa kesho Jumanne Julai 9, 2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam Media, waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo na Charles Wandwi.


Post a Comment

0 Comments