Mara baada ya klabu ya Everton kuwafunga mabingwa wa Sportpesa Super Cup, Gor Mahia kwa jumla ya magoli 2-1 mchezo uliyochezwa Julai 13 katika uwanja wa taifa jiji Dar es salaam timu hiyo ya Uingereza imeendeleza vipigo katika michezo yake ya kirafiki.
Everton imeifunga klabu ya FC Twente ya nchini Uholanzi kwa jumla ya magoli 3-0.
Wachezaji ambao wameonekana kuwa mwiba mchungu mbele ya kikosi cha FC Twente ni Kevin Mirallas, Aaron Lennon na Kieron huo huku Wayne Rooney akiendelea kuwa kivutio.
Picha zikionyesha matukio ya uwanjani
0 Comments