Makamba atengua uteuzi wa wajumbe saba NEMC

Makamba atengua uteuzi wa wajumbe saba NEMC


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba ametengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa makosa mbalimbali ikiwamo kushindwa kutatua changamoto kikamilifu na kwa wakati.

Akizungumza leo Jumatatu, Julai 17, Makamba amesema licha ya unyeti wa taasisi hiyo katika kuharakisha azma ya Serikali katika ujenzi wa viwanda bado baraza hilo limekuwa na utendaji wa kusuasua hususani katika kuchelewesha vyeti vya ukaguzi wa tathimini ya mazingira kwa wawekezaji.

Amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita wizara ilikuwa ikifanya uchunguzi kubaini utendaji wa mamlaka hiyo na kwa bahati mbaya utendaji huo haukuwa sawa.

"Kwa sasa umuhimu wa NEMC ni mkubwa mno kuliko miaka yote hivyo inapogundulika kuwa kuna utendaji usioridhisha lazima hatua zichukuliwe kwa mamlaka nilionayo kisheria,"alisema.

Post a Comment

0 Comments