Watakaojitangazia matokeo Kenya kukiona

Watakaojitangazia matokeo Kenya kukiona


Nairobi, Kenya. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini kenya (CA), Francis Wangusi, amewataka wanasiasa wasithubutu kutangaza matokeo ya uchaguzi sambamba na Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwani hilo linaweza kusababisha machafuko.

Amewaonya wanasiasa hao kuwa atakayefaya hivyo atakabiliwa na hatua kali za kisheria.

Onyo hilo limewalenga makamanda wa muungano wa Nasa ambao wameahidi kwamba watakuwa na mfumo wao wa kupokea, kujumlisha na kutangaza matokeo ya urais mara vituo vya kupigia kura vitakapofungwa saa 12.00 jioni.

Hatua hiyo ya Nasa ni tofauti na msimamo wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC) ambayo imepanga kutangaza matokeo yote ya urais baada ya siku saba.

Wangusi amewaambia wanahabari: "IEBC pekee ndio wanaruhusiwa na sheria kutangaza matokeo. Wengine wanaweza kufanya hivyo baada ya IEBC."

Mkurugenzi huyo mkuu wa mamlaka ya mawasiliano aliongeza kwamba wanafahamu kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinapanga kutoa matokeo kabla ya tume.

“Tunavifahamisha vyombo vyote vya habari vinavyofanyia mzaha wa kutangaza matokeo kabla ya IEBC kuacha mara moja. IEBC ndiyo chombo pekee rasmi kilichopewa jukumu la kutangaza matokeo.”

Post a Comment

0 Comments