Urusi yajipanga kulipa kisasi Marekani

Urusi yajipanga kulipa kisasi Marekani


 Ofisa mwandamizi katika Ikulu ya Kremlin amesema Urusi inalazimika kulipiza kisasi kwa hatua ya Marekani kushikilia mali za wanadplomasia waliofukuzwa mwaka jana kwa madai ya kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani.

Konstantin Kosachev alisema jana kwamba licha ya kuwatimua wanadiplomasia mwaka jana, Marekani bado inashikilia majengo mawili ya maofisa hao.

"Katika mazingira haya, sasa inaonekana Urusi haina chaguo: ni wakati wa kulipiza kisasi. Hili halitakuwa chaguo letu na hizi zitakuwa hatua za kushurutishwa, lakini lazima zifuatwe,” alisema Kosachev.

Kosachev alisisitiza kwamba kauli iliyotolewa na Ikulu ya White House ni uthibitisho wa Marekani wa kutoheshimu sheria za kimataifa na akataja kuwa ni "jaribio la kukuza dhana ya sheria za taifa kwanza dhidi ya zile za kimataifa."

Post a Comment

0 Comments