Darasa la 7 Wamponza Godbless Lema ........Apigwa marufuku kufanya Mkutano

Darasa la 7 Wamponza Godbless Lema ........Apigwa marufuku kufanya Mkutano



Jeshi la Polisi mkoani Arusha limepiga marufuku mikutano ya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema iliyokuwa ianze jana kwa maelezo kuwa kuna maandalizi ya mtihani wa darasa la saba na mbio za Mwenge wa Uhuru.

Taarifa kutoka Ofisi ya Mkuu wa polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) E.Tille wilayani Arusha, amesema katika barua yake iliyothibitishwa na Kamanda wa polisi Arusha, Charles Mkumbo imesema kuwa Mhe. Lema amezuiwa kufanya mikutano iliyokuwa imepangwa kuanzia jana hadi Septemba Mosi.


“Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha inakutaarifu kuwa imezuia mikutano yako yenye ratiba kuanzia Agosti 27 hadi Septemba 1 kwa ajili ya kupisha maandalizi ya kuhitimisha mtihani wa darasa la saba na Mwenge wa Uhuru,” Sehemu ya barua hiyo ilinukuliwa.


Kamanda Mkumbo alisema sababu ya kuzuia mikutano hiyo ni polisi kuhitajika kwa ulinzi, hivyo haiwezekani kupata wa kulinda mikutano na kushiriki masuala ya mitihani na Mwenge.


“Haya ni mambo ya kitaifa, hivyo ndiyo sababu OCD amesitisha mikutano ya mbunge na mambo haya yakimalizika ataendelea na mikutano yake,” alisema.

Post a Comment

0 Comments