Ushawahi kufikiria kuwa mtoto wa rapper Kanye West, North West kuna ngoma anaizimia kutoka kwa baba yake?
Kama ulikuwa haufahamu, basi ni kwamba mtoto huyo mwenye miaka minne anaizimia ngoma moja tu ya baba yake ambayo ni ‘Amazing’ ambayo alishirikishwa Young Jeezy.
Ngoma ya Amaizing, ilitoka mnao mwaka 2009 ikiwa katika albamu ya 808s & Heartbreak classic.
Pia North hakuacha kutaja msosi anaopenda kula mara kwa mara ambao ni Pizza na anapenda kutazama kipindi cha ‘Shimmer and Shine’ katika runinga na rangi anayopenda ni ‘Rainbow’.
North na Mama yake wanatarajiwa ku-Cover jarida la Interview Magazine, ambapo Kim ataongelea kuhusu TV-Show yake ya Keeping Up with the Kardashians na mipango ya Yeezy. Vile vile inadaiwa huwenda atagusia kuhusu ujauzito aliobeba mtu waliyemlipa kwa ajili ya mtoto wao wa tatu.
0 Comments