Mtu anayefanya biashara ya dawa za kulevya anahusika na rushwa – Rais Magufuli

Mtu anayefanya biashara ya dawa za kulevya anahusika na rushwa – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu anayefanya biashara ya dawa za kulevya kwa vyovyote vile anahusika na rushwa.


Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa TAKUKURU katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

“Nataka chombo hichi cha TAKUKURU cha Tanzania nataka kifanye kama wanavyofanya wengine, msiwe na kigugumizi kwa kitu mlichokuwa na ushahidi na nyinyi msije mkawa party ya kudivert masuala ambayo yako wazi, chombo hichi kila mahali unapotaka kuplay party una play hata kama ni biashara ya madawa ya kulevya mtu anaefanya biashara ya madawa ya kulevya kwa vyovyote anahusika na rushwa,” alisema Rais Magufuli.

“Nilazima amewahonga watu, amedanganya watu kwa kumeza madawa hayo, ndugu Mkurugenzi nasema haya sitaki kuwa mnafki nataka niwaeleze ukweli changamoto zipo, je? changamoto zilizo katika kazi zenu je mnazishughulikia vizuri ,je mnajipangaje katika masuala mabyo ni muhimu investigation na mahali pengine, je anaefanya investigation qualification zake ni nzuri zinafaa kwa investigations.”

Hata hivyo Rais Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi hiyo kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Post a Comment

0 Comments