Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zuberi anafanya mazungumzo na waumini waliokwama kusafiri kwenda kufanya ibada ya hija Makka, Saudi Arabia.
Waumini hao takriban 100 walikwama kusafiri Agosti 23 baada ya taasisi iliyoandaa na kuratibu safari yao kuelezwa kuwafanyia udanganyifu na kuchukua fedha zao.
Kikao hicho kimedumu kwa zaidi ya saa mbili sasa kikielezwa kuwa kinalenga kupata ufafanuzi wa tuhuma zinazoikabili taasisi hiyo yenye ofisi zake Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Waumini hao walisema taasisi hiyo ilikusanya fedha takriban Sh10 milioni kutoka kwa kila muumini kwa ajili ya safari hiyo.
0 Comments