Mwanafunzi atoweka katika mazingira tata

Mwanafunzi atoweka katika mazingira tata


Dar es Salaam. Mtoto mwenye miaka saba, Musa Tano amepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Jumatatu (Agosti 28) akiwa nyumbani kwao Kidaraja cha Chuma, eneo la Tabata Kisiwani wilayani Ilala.
Akizungumza na MCL Digital, shangazi wa mtoto huyo Waridi Mnyime amesema Musa alipotea saa nane mchana alipokuwa akicheza na wenzake nyumbani kwao katika Mtaa wa Twiga.
Mnyime amesema wameshatoa taarifa polisi ambako wamepewa RB namba TBWRB/162/2017.
"Wakati anapotea alikuwa amevaa sweta la mikono mirefu lenye mistari ya bluu bahari na nyeupe na suruali ya jeans rangi ya bluu," amesema.
Amesema Musa ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Makuburi Jeshini.
Mnyime amesema atakayemwona atoe taarifa kituo chochote cha polisi au apige simu namba 0653 985 587.


Post a Comment

0 Comments