Kocha wa klabu ya Mbeya City, Kinnah Phiri amepiga hodi katika ofisi za Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia kupeleka malalamiko yake ya mishahara ya miezi minne anayodai, huku akiwa njia panda kuhusu ajira yake.
Kinnah Phiri
Phiri ambaye yupo jijini Mbeya awali alikuwa anadai mishahara ya miezi mitano na kila mwezi analipwa Tsh milioni 6.5 na mpaka sasa amelipwa mshahara wa mwezi mmoja, huku akipigwa danadana ya kumaliziwa fedha yake.
“Hapa kwanza wanilipe mishahara yangu iliyobaki ambapo nimewasiliana na Rais wa TFF Karia ameahidi kunisaidia na amesema Jumatatu (leo) atanipa jibu jinsi walivyowasiliana na viongozi wa Mbeya, japo wanaweza kukatwa kwenye pesa zao za udhamini ama mapato ya getini kama TFF wataamua kunisaidia kwa kunilipa wao, Hapa sio kwetu, naishi katika mazingira magumu, nikimaliza hili itabidi nifungue kesi FIFA juu ya mkataba wangu uliovunjwa bila makubaliano yoyote na mimi, “amesema Phiri aliyebakisha miezi 18 katika mkataba wake na Mbeya City kwenye mahojiano na gazeti la Mwanaspoti.
Hata hivyo, Uongozi wa Mbeya City unashindwa kufafanua lolote juu ya Phiri zaidi ya kusisitiza bado ni kocha wao ingawa hayupo na timu yao iliyoshinda mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Majimaji kwa bao 1-0.
0 Comments