Serikali yawakaribisha vijana kutoa mawazo

Serikali yawakaribisha vijana kutoa mawazo


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama 

Dar es Salaam. Serikali imekamilisha uandaaji wa kanuni kwa ajili ya kuanzisha Baraza la Vijana nchini, ambalo litatoa fursa kwa vijana kuwasilisha mawazo yao moja kwa moja serikalini.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema uandaaji wa kanuni hizo umekamilika na kwamba, baraza hilo litaanza kazi wakati wowote kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa. Mhagama alisema lengo la kuanzishwa kwa baraza hilo ni kuwaunganisha vijana wote wawe karibu na Serikali.


“Serikali ipo tayari kuwasililiza vijana iwapo wataonyesha juhudi za kutafuta fursa za ajira, badala ya kuzisubiri ziwafuate,” alisema.


Alibainisha kuwa utafiti wa nguvu kazi uliofanywa nchini mwaka 2014, ulionyesha watu milioni 25 sawa na asilimia 56 ndiyo wenye uwezo wa kufanya kazi kati ya watu watu 44 milioni.


Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Maambukizi ya Ukimwi (TacAids), Jumanne Issango alisema maambukizi mapya ya VVU yanaongezeka lakini kupitia mkutano huo watajadili namna ya kukabiliana nayo na kuweka mikakati ya kuhakikisha vijana wanajiepusha na janga hilo.


Naye, Makamu wa Rais wa Shirika la Global Health nchini Marekani, Robert Clay alisema fursa waliyoipata vijana waitumie vizuri kutoa mawazo yenye tija yatakayosaidia kupanga mikakati ya kuboresha ajira


Post a Comment

0 Comments