Kwa sasa Cesar Azpillicueta na Alvaro Morata ndio combination hatari kuliko yoyote barani Ulaya

Kwa sasa Cesar Azpillicueta na Alvaro Morata ndio combination hatari kuliko yoyote barani Ulaya


Hii leo mtaani mashabiki wa Chelsea wanatembea vifua mbele baada ya hapo jana Alvaro Morata kuionesha dunia ni nini amekuja kufanya Uingereza na kuwanyamazisha waliokuwa wanamsema.

Tayari Conte amemwagia sifa nyingi mshambuliaji huyo na kusema kwamba ni kijana mzuri sana kiasi kwamba hata kama una binti unataka muoezesha baasi muozeshe kwa Alvaro, lakini kuna mambo yafuatayo ya kufahamu kutokana na ushindi wa jana wa Chelsea.

Alvaro Morata alifunga hat trick yake ya kwanza, lakini je unajua ya kwamba hat trick hii ya Morata imechukua muda mrefu tofauti na Diego Costa. Diego Costa yeye alitumia mechi 4 tu kufunga hat trick huku Morata akitumia 6.

Wakati Morata akifanya hivyo, mchezaji mwingine mpya Chelsea Tiemoue Bakayoko yeye kwa siku ya jana alifanya tackle zilizofanikiwa 5, hiyo ni idadi ambayo jana katika michezo yote hakuna kiungo aliyemzida kwa tackling.

Chelsea hapo hapo, baada ya magoli matatu ya jana ya Morata inawafanya Chelsea kwa sasa mabao 10 kati ya 13 waliyofunga msimu huu yamefungwa na watu wa taifa moja la Hisapania.

Lakini vile vile kama hujui tu ni kwamba katika ligi 4 kubwa barani Ulaya hakuna Combination ambayo imezalisha mabao mengi hadi sasa kama combination ya Alvaro Morata na Cesar Azipiculeta, hadi sasa wametengeneza mabao manne.

Post a Comment

0 Comments