Messi afunga bao la 100

Messi afunga bao la 100


Messi afunga bao la 100, huku Barcelona ikiilaza Olympiakos

Lionel Messi alifunga bao lake la 100 barani Ulaya huku Barcelona ikifanya mechi hiyo kuwa rahisi licha ya kadi nyekundu aliyopewa Gerard Pique na kuilaza Olympiakos katika kombe la vilabu bingwa.

Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 30 alifunga mkwaju wa adhabu na kuwanyamazisha wenyeji wao baada ya mchezaji wa timu hiyo Dimitris Nikolaou kujifunga mapema.

Messi baadaye alimpatia pasi Lucas Digne aliyefunga bao la tatu kabla ya kichwa kizuri cha Nikolaou kupata bao la kufutia machozi.

Pique alipewa kadi ya pili ya njano baada ya kuunawa mpira.

Beki huyo wa kati alitumia mkono wake kuuweka mpira katika eneo hatari baada ya shambulio la Gerard Deulofeu kupanguliwa na kumrudia yeye.

Post a Comment

0 Comments