BREAKING: Wema aachiwa huru na mahakama, Wakili wake awaonya wasanii juu ya matumizi ya madawa ya kulevya (+video)

BREAKING: Wema aachiwa huru na mahakama, Wakili wake awaonya wasanii juu ya matumizi ya madawa ya kulevya (+video)





Wakili wa Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu, Alberto Msando amesema kuwa tayari mteja wake ameshalipa faini ya milioni 2 na ameshakuwa mtu huru. Hii ni baada ya asubuhi ya leo Mahakama ya Mkazi Kisutu kumhukumu msanii huyo kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya milioni 2 kwa kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi madawa ya kulevya aina ya bangi nyumbani kwake.






Msando akiongea na waandishi wa habari mapema mchana wa leo Julai 20, 2018 nje ya mahakama baada ya hukumu hiyo kutolewa, amesema kuwa huu ni muda kwa wasanii wote kujitathmini kwani wengi wao wamekuwa wakitumia madawa ya kulevya jambo ambalo linaua vipaji vyao na kuharibu jamii kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments