Ferguson aweka wazi hali yake ya kiafya kwa sasa

Ferguson aweka wazi hali yake ya kiafya kwa sasa


Meneja wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ameonekana kwa mara ya kwanza mbele ya jamii akizungumza tangu alipofanyiwa upasuaji wa Ubongo.

Sir Alex Ferguson (76) amewashukuru wote waliompa sapoti katika kipindi chote alichokuwa hospitali na kuahidi kuwa ataanza kuhudhuria mechi za Manchester United hivi karibuni.

“ Hello, huu ni ujumbe wangu wa haraka kwenu, kwanza kabla ya yote napenda niwashukuru jopo la madaktari wa hospitali ya Macclesfield, Salford Royal na Alexandra kwani bila ya wao kuonesha kunijali kwa kiwango kikubwa nisingelionekana hapa leo “. Amesema Sir Alex Ferguson.

“ Jumbe zote za kunitakia afya njema nilizopokea kutoka sehemu mbalimbali Duniani zimenifanya niwe mnyenyekevu na kuwashukuru kwa sapoti, lakini mwisho niwaahidi nitarejea uwanjani baadae msimu huu kuiangalia timu na namtakia kila laheri Jose na wachezaji “. Ameongeza.

Wachezaji kadhaa ambao aliwahi kuwafundisha katika klabu hiyo wakiwemo, Wayne Rooney na Edwin Van der Sar kupitia kurasa zao za Twitter, wamepokea kwa furaha ujumbe huo na kumtakia mapumziko mema.

Ferguson alistaafu kufundisha soka mwaka 2013, baada ya kuingoza Manchester United kwa miaka 27 lakini licha ya kustaafu ameendelea kuhudhuria mechi mbalimbali za klabu hiyo.

Kocha huyo aliyejiunga United mwaka 1986 akitokea klabu ya Aberdeen ya Scotland amebaki kuwa ni kocha pekee katika visiwa vya Uingereza mwenye mafanikio makubwa, akiwa ameshinda mataji 49 ambapo 38 kati ya hayo ameshinda akiwa Man United.


ad

Post a Comment

0 Comments