Huyu ndio msaidizi mpya wa Maurizio Sarri Chelsea

Huyu ndio msaidizi mpya wa Maurizio Sarri Chelsea

Huyu ndio msaidizi mpya wa Maurizio Sarri Chelsea

Klabu ya Chelsea hivi karibuni imemtambulisha kocha wake mpya anayejulikana kwa jina la Maurizio Sarri akijiunga na wababe hao wa Darajani akitokea katika klabu ya Napoli ya nchini Italia.


Sarri ametambulishwa Chelsea kuchukua nafasi ya Muitaliano mwenzake Antonio Conte aliyetimuliwa baada ya mwenendo mbaya wa klabu hiyo.

Licha ya kutambulishwa rasmi kama kocha mkuu ameamua kumteua Gianfranco Zola kama msaidizi wake,Zola wakati wa karia yake aliwahi kuitumikia Chelsea kwa takribani miaka 7 kuanzia mwaka 1996 hadi 2003,lakini pia aliwahi kuichezea Napoli kuanzi 1989-1993 klabu ambayo ametoka Maurizio Sarri.


Gianfranco Zola kabla ya kujiunga na Chelsea kama kocha msaidizi alikuwa akiinoa klabu ya Birmingam City ambayo alianza kuifundisha kuanzia mwaka 2016/17.


Licha ya kuifundisha Birmingham City aliwahi kuvifundisha baadhi ya vilabu nchini Uingereza vikiwemo West Ham,Watford,pia timu ya taifa ya Italia chini ya miaka 16 kuanzia mwaka 2011/12.

Post a Comment

0 Comments