Haji Manara adai Yanga wameifedhehesha Tanzania, amtaka Rais Magufuli aingilie kati
Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amedai kuwa klabu ya Yanga imeifedhehesha Tanzania nchini Kenya usiku wa kuamkia leo kwa kukubali kipigo cha goli 4-0.
Haji Manara
Manara akikazia hoja yake amesema Yanga wanatumia fedha nyingi za kigeni hovyo kwa miaka yote jambo ambalo halileti maana kwani klabu hiyo imekuwa ikivurunda kwenye michuano ya kimataifa huku akimuomba Rais Magufuli aingilie kati matumizi hayo mabovu ya fedha ndani ya klabu hiyo.
“Mhe. Rais wangu wakati huu ukikimbizana na ujenzi wa Viwanda nchini na kuinua Uchumi wetu..nakuomba pia utupie jicho na huku..kuna klabu kwa miaka yote imekuwa ikitumia hovyo fedha za kigeni na kulitia aibu Taifa letu leo Wameifedhehesha Nchi.“ameandika Manara kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Klabu ya Yanga jana imekubali kipigo cha mbwa koko cha goli 4-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kwenye mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
0 Comments