Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Seleman Kakoso (wa tatu kulia), akishirikiana na Naibu Waziiri wa Miundombinu, Mhe Eng Atashasta Ndikiye (katikati aliyevaa kofia), Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, viongozi wa serikali, pamoja na wakurugenzi wa kampuni ya simu ya Tigo na Mfuko wa Kudumu wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kukata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa mawasiliano uliojengwa na UCSAF na Tigo ili kuwezesha mawasiliano ya simu kwa mara ya kwanza katika kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro juzi.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Dk Joseph Kilongola akitoa risala zake wakati wa hafla ya uzinduzi wa minara ya simu itakayowezesha upatikanaji wa mawasilino kwa mara ya kwanza katika kata za Kumbulu, Balama na Nongwe, WIlaya ya Gairo Mkoani Morogoro. Minara hiyo ilijengwa kwa ushirikiano baina ya Tigo na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuzinduliwa jana na wahemshimiwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Mawasiliano ya Bunge.
Wananchi wa Kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakicheza kwa furaha pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge – Miundombinu, Mhe mbunge Rashid Mohammed Chwachwa (Masasi- aliyejifunga shuka) wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo.
Wananchi wa Kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakicheza kwa furaha pamoja na Naibu Waziri wa Miundombinu – Mhe Eng Atashasta Ndikiye (katikati aliyevaa kofia) wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo.
Wananchi wa Kata ya Kumbulu, Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro wakiigiza adha walizokuwa wanazipata kupata mawasiliano ya uhakika ya simu wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo unaowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza katika kata hiyo. Mnara huo pamoja na mingine katika kata za Balama na Nongwe ilijengwa kwa ushirikiano baina ya Tigo na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuzinduliwa na wahemshimiwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Mawasiliano ya Bunge.
Ikiwa sehemu ya juhudi zake kuhakikisha kuwa kila mtu anashiriki kukuza uchumi wan chi na kupata maendeleo yatokanayo na huduma bora za mawasiliano, kampuni ya Tigo Tanzania imepanua mtandao wake katika maeneo ya pembezoni katika kata za Kumbulu and Balama yaliyopo wilaya ya Gairo, Mkoani Morogoro.
Akizindua minara hiyo mipya inayowezesha mawasiliano ya simu kupatikana kwa mara ya kwanza kabisa katika kata hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu. Mheshimiwa Seleman Kakoso alisema kuwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano huleta mabadiliko makubwa ya ukuaji wa uchumi, ubunifu na maisha ya watu kwa ujumla. Mhe Kakoso alimbatana na Naibu Waziri wa Miundombinu, Mhe Eng. Atashasta Ndikiye, waheshimiwa wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu pamoja na viongozi wengine wa serikali.
‘Nawashukuru Tigo kwa kuitikia mwito wa Serikali na kushiriki kikamilifu katika kuunganisha maeneo haya ya pembezoni ambayo hapo zamani hayakuwa na mawasiliano yoyote ya simu kwa sababu hayana mvuto mkubwa wa kibiashara. Ninatoa wito kwa kampuni nyingine za simu kuiga mfano huu ili kuhakikisha kuwa kila mtu anapata fursa ya kuwa sehemu ya mageuzi makubwa yatokanayo na Tehama, huku wakizingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali katika kutimiza miradi ya aina hii,’ alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Dk Joseph Kilongola alibainisha kuwa minara hiyo ilikuwa imejengwa kwa ushirikiano baina ya UCSAF na Tigo kama sehemu ya zabuni ya zinazolenga kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha mawasiliano ya uhakika kwa wananchi wote.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa alisema kuwa lengo kuu la Tigo ni kuwaunganisha Watanzania zaidi ya milioni 13 ambao kufikia sasa bado hawana huduma za mawasiliano.
‘Tigo inaamini kuwa upatikanaji wa mawasiliano utaibua fursa mpya za kiuchumi, elimu, afya, biashara na kubadili maisha ya watu,’ alisema. Mutalemwa alisema kuwa kampuni ya Tigo imelenga kuunga mkono juhudi za serikali za kujenga Tanzania ya viwanda kwa kupanua mtandao wake ili kuwezesha nchi nzima kufurahia faida za utandawazi utakanao na mawasiliano ya uhakika.
“Tunafuhari kuwa Serikali imetambua tofauti kubwa ya upatikanaji wa mawasilaino iliyopo baina ya maeneoa ya mijini na vijijini, na kujitolea kwake kufadhili zabuni mbali mbali zinazowezesha kampuni za simu kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo mbali mbali kama kata hizi za Balama, Kumbulu na Nongwe ambazo hapo awali hazikuwa na huduma yoyote ya mawasiliano ya simu kwa sababu hazina mvuto mkubwa wa biashara,’ alisema.
Tigo imeshiriki katika zabuni za UCSAF tangu mwaka 2012 ambapo kufikia sasa imefanikiwa kushinda zabuni zilizoiwezesha kuunganisha zaidi ya kata 100 na huduma za mawasiliano.
0 Comments