Matola atoa kauli yake juu ya kipigo cha Yanga

Matola atoa kauli yake juu ya kipigo cha Yanga


BAADA ya Yanga kuambulia kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Gor Mahia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, juzi Jumatano, aliyewahi kuwa kocha wa Simba ambaye kwa sasa anainoa Lipuli, Seleman Matola amefunguka kuwa matokeo hayo siyo ya kushitua.

Yanga tangu ianze kucheza kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo, haijafanikiwa kushinda mchezo hata mmoja katika michezo yake mitatu ambapo bado inaburuza mkia kwenye Kundi D ambalo lina timu za USM Alger, Rayon Sports na Gor Mahia.

Matola amesema matokeo ambayo Yanga wameyapata, watu wengi hawajashituka na hii ni kutokana na kile ambacho kinaendelea ndani ya klabu hiyo kwa sasa hasa suala la uchumi.

Kocha huyo alisema kuwa, Yanga walitakiwa kuwa makini na kupambana kwa hali yote kwa sababu wanawakilisha nchi na kusahau matatizo yao.
“Ule mchezo ulikuwa ni mgumu kwao kushinda na matokeo yake ndiyo maana watu wengi hawajashituka kutokana na hali halisi ambayo inawakabili ingawa walipaswa kupambana kwa sababu walikuwa wanawakilisha nchi na si vinginevyo,” alisema Matola.

Post a Comment

0 Comments