Mbunge Ester Mahawe Awashangaa Wapinzani

Mbunge Ester Mahawe Awashangaa Wapinzani



Na John Walter Babati
Mbunge wa viti maalum Ccm mkoa wa Manyara mheshimiwa Ester Mahawe amesema anashaangazwa na upinzani kusimama majukwaani na kusema serikali haifanyi kazi.


Ameyasema hayo wakati akimnadi mgombea udiwani wa chama hicho katika kata ya Bagara Nikodemus Bonifasi [Nyeusi] katika mtaa wa Osterbay mjini Babati leo.


Amesema serikali iliyopo madarakani imefanya mengi na itaendelea kufanya,akitolea mfano ndege saba ambazo serikali imenunua kwa pesa za ndani ili kuinua shirika la ndege [ATCL] na kuongeza kasi ya uchumi wa nchi pamoja na barabara za lami zinazoendelea kujengwa mjini Babati kilomita kumi.


Mgombea udiwani wa Chama cha Mapinduzi [CCM] Nikodemus Bonifasi amesema kuwa kwake yeye udiwani si kitu,bali anaangalia wananchi wanataka nini.


Akizungumzia mambo ambayo atayafanya endapo wananchi wa kata ya Bagara watampatia nafasi amesema tayari chama chake kimeshaorodhesha katika ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015,’Kwa hiyo mimi nitakachokifanya ni kusimamia utekelezaji” alisema Nyeusi.


Akieleza kwanini aliondoka Chadema alisema ameondoka kwa sababu Chadema wanapinga kila jambo linalofanywa na serikali na kwamba yeye chama hicho hakina mkataba na wananchi bali CCM ndio kina mkataba na wananchi wake.


Kwa upande wa mgombea wa Chadema Mathias Zebedayo amewaambi wakazi wa kata ya Bagara kuwa akipata nafasi ya kuwa diwani atahangaika kuhakikisha Mbaazi na Mahindi yanapanda bei pamoja na kusimamia upimaji wa maeneo ambayo hayajapimwa katika kata hiyo.
ad

Post a Comment

0 Comments