Mshambuliaji Alexis Sanchez
KOCHA Jose Mourinho amekiri kuwa kumkosa mshambuliaji wake, Alexis Sanchez kwa siku 20 ni pigo kubwa katika kikosi chake wakati huu ambapo kipo kwenye ziara nchini Marekani.
Sanchez alizuiliwa kuingia nchini humo akiwa na kikosi cha Manchester United kutokana na tatizo la Visa lililotokana na rekodi za nyuma za mchezaji huyo kutolipa kodi miaka ya nyuma akiwa nchini Hispania.
Mourinho amekiri kuwa kutokuwa na staa huyo ambaye pia alikuwa katika mapumziko ya muda mrefu kwa kukosa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kuna mpa hofu juu ya ufiti wake.
“Sijui kama ataweza kujiunga na sisi, hii ni habari mbaya kwetu, kwake na kwa timu kwa jumla, hata kwa waratibu wa michuano ya huku (Marekani) siyo nzuri.
“Lakini hakuna wa kumlaumu, klabu inafanya kazi kubwa na nina heshimu mamlaka za Marekani na litakuwa jambo la muhimu kufanya kazi na (Anthony) Martial, Alexis na (Juan) Mata ambao ni wachezaji tulionao kwenye idara ya ushambuliaji.
“Hatuna (Romelu) Lukaku, (Jesse) Lingard, Marcus Rashford, ndiyo maana nasema Alexis akikosekana kwa siku 20 ni jambo bay asana,” alisema kocha huyo.
RATIBA YA ZIARA YA MAN UNITED
Julai 20 – Club America
Julai 22 – San Jose Earthquakes
Julai 25 – AC Milan
Julai 28 – Liverpool
Julai 30 – Real Madrid
0 Comments