Louis Vuitton ni kampuni ya fashion ya Ufaransa ilioanzishwa mwaka 1854 na mwanamitindo maarufu Louis Vuitton na kampuni hiyo ni maarufu kwa kutengeneza vitu mbalimbali kama bags, viatu, nguo, accessories, miwani na mpaka vitabu.
Kampuni ya LV iliwahi kutajwa kama kampuni namba moja kwa utengenezaji wa vitu vyenye thamani ya juu zaidi duniani na bado haijaacha kubuni vitu vya kitofauti na vyenye gharama ya juu zaidi ambapo mwaka huu wa 2018 wamezindua choo cha kukaa cha brand ya Louis Vuitton chenye thamani ya Dola 100,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Shillingi Milioni 220 za Kitanzania.
Louis Vuitton ni moja kati ya kampuni kubwa za fashion duniani na kwa miaka sita mfululizo kuanzia 2006 hadi 2012 kampuni hiyo ya Louis Vuitton ilitajwa kama kampuni namba moja kwa utengenezaji wa vitu vyenye thamani ya juu zaidi.
Pia kwa mwaka huu 2018 Louis Vuitton ndio kampuni pekee iliyokuwa imepewa nafasi ya kutengeneza begi maalum la kubebea Kombe la Dunia lililofanyika nchini Urusi.
0 Comments