Rais Kiir akubali yaishe, kuunda Serikali ya Umoja wa Kimataifa

Rais Kiir akubali yaishe, kuunda Serikali ya Umoja wa Kimataifa


Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesema yuko tayari kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayojumuisha pande zote kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya pande husika.

Amesema yuko tayari kufanya hivyo ili kuhitimisha mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika ambao umekwamisha juhudi za maendeleo.

Uamuzi huo wa Rais KIIR umekuja baada Wizara ya Mambo ya Nje Sudan imesema pande hasimu nchini Sudan Kusini zimefikia makubaliano ya kugawana madaraka ambayo yaliyotarajiwa kutiwa saini jana.

Nchi hiyo, ambayo ilijitenga na Sudan mwaka 2011, ilitumbukia katika vita vya ndani baada ya Rais SALVA KIIR kumtuhumu aliyekuwa makamu wake RIEK MACHAR kuwa alihusika na jaribio la kuipindua serikali yake.

Post a Comment

0 Comments