Shilole awafungukia Wanawake wanaopenda kuishi maisha ya kudanga

Shilole awafungukia Wanawake wanaopenda kuishi maisha ya kudanga


Mwanamuziki wa kizazi kipya shilole awatolea uvivu wanawake wanaopenda kuishi maisha ya kudanga na wale wanaojigamba kuwa masupastaa lakini hawana pa kulala.

Shilole ameongea hayo wakati alipofanyiwa mahojiano na wasafi TV na kutoa yake ya moyoni kuhusu tabia mbaya wanazozifanya wanawake wengi wa mjini ili maisha yao yawaendee vizuri.

" Mwanamke inabidi ujitambue heshimu thamani yako we ni nani sio kudanga na wanaume kibao wakati hao wanaume wakikutana wanaambiana tayali nishapita pale jana mwanamke mwanamke wa kudanga ni mfu Mtarajiwa akijiheshimu ataheshimiwa " alisema shilole

"Uwezi kuwa supastaa ukawa hauna pa kuishi, huna gari na anamaisha yake uwezi kujiita supastaa wa instagram wakati pa kuishi ni shida mimi naweza kusema naweza kulala popote hata kama kwenye gari lakini nina nyumba yangu majohe ambapo muda wowote naweza kwenda"

Post a Comment

0 Comments