Mchezaji Yanga: Mshahara wasababisha Yanga kufungwa bao 4

Mchezaji Yanga: Mshahara wasababisha Yanga kufungwa bao 4


Straika hatari wa zamani aliyewahi kuichezea Yanga, Mkenya, Boniface Ambani, amesema kiwango cha timu hiyo namna ilivyocheza dhidi ya Gor Mahia FC haukuwa unaendana na ukubwa wa klabu.

Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Jumatano ya wiki hii jijini Nairobi, Kenya, Yanga waliruhusu nyavu zao kutikishwa mara nne bila majibu na Gor Mahia ambao ni mabingwa watetezi wa ligi nchini humo.

Kwa mujibu wa Radio EFM, Ambani ameeleza kuwa Yanga haikuonesha kiwango kinachoendana na ukubwa wa klabu na inapaswa kufanya usajili wa maana ili kuepusha aibu.

Ambani ambaye aliwahi kutamba na Yanga miaka ya 2000 akiwa kwenye kikosi hicho mwaka 2009 amesema kikosi kinapaswa kufanyiwa maboresho tofauti na wachezaji aliowaona kutokuwa na uwezo wa kutosha.

Mbali na uwezo, Ambani amefunguka kuwa aliongea na baadhi ya viongozi wa Yanga na wakamdokezea kuwa wachezaji hawajalipwa mshahara, jambo ambalo linaweza likawa limepelekea kuambulia kichapo hicho cha mchezo wa mkondo wa kwanza.

Ambani amesema aliambiwa wachezaji kadhaa bado hawajpokea stahiki zao huku wengine wakibaki Dar es Salaam wakigomea kusafiri wakiomba kuongezewa mikataba mingine ili waendelee kuichezea timu.

Hassan Kessy na Kelvin Yondani ni wachezaji waliobaki nchini wakati kikosi cha Yanga kikisafiri kuelekea Kenya kwa ajili ya mchezo dhidi ya Gor Mahia.

Post a Comment

0 Comments