Dkt. Shein akutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jimbo la Gorontalo na Kiongozi wa Kampuni ya gesi nchini Indonesia

Dkt. Shein akutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jimbo la Gorontalo na Kiongozi wa Kampuni ya gesi nchini Indonesia


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amefanya mazungumzo na Makamo wa Rais wa Indonesia Muhammad Jusuf Kalla ambapo katika mazungumzo hayo viongozi hao walisisitiza haja ya kuzidisha ushirikiano katika sekta za maendeleo.


Viongozi hao walifanya mazungumzo katika Ofisi ya Makamo wa Rais wa Indonesia Muhammad Jusuf Kalla iliyopo mjini Jakarta Indonesia, ambapo mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mawaziri wa pande zote mbili. 


Katika mazungumzo hayo Rais Dk. Shein alimpongeza Makamo wa Rais wa nchi hiyo kwa muwaliko wake huo muhimu ambao unaimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Indonesia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla na makhsusi kwa Zanzibar. 


Dk. Shein alimueleza Makamo huyo wa Rais wa Indonesia kuwa Tanzania inajivunia kwa kiasi kikubwa uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya pande mbili hizo ambao umeasisiwa na viongozi wakuu wa nchi hizo tokea miaka ya sitini na kuahidi kuwa utaendelezwa. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Meya wa Jimbo la Gorontalo Prof.Nelson Pamalingo wakati wa mkutano na Meya huyo yaliyogusia zaidi katika ushikiano wa kilimo cha Minazi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Borobudur Mjini Jakarta, Indonesia katika ziara ya kikazi kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) na Ujumbe wake katika mazungumzo na Meya wa Jimbo la Gorontalo Prof. Nelson Pamalingo (kulia) wakati wa mkutano na Meya huyo yaliyogusia zaidi katika ushikiano wa kilimo cha Minazi hafla ya mazungumzo hayo ilifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Borobudur Mjini Jakarta,Indonesia katika ziara ya kikazi kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Meya wa Jimbo la Gorontalo Prof.Nelson Pamalingo(katikati) na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi katika Ujumbe wake Rais (kushoto) na Viongozi waliuongama na Mstahiki Meya wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya mazungungumzo ya pamoja yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Borobudur Mjini Jakarta,Indonesia katika ziara ya kikazi kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Kiongozi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Pertamina ya Jakarta Nchini Indonesia Bw.Daniel S.Purba akiwa na ujumbe wa kampuni hiyo walipofika kwa mazungumzo katika ukumbi wa Ofisi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN) Mjini Jakarta Indonesia Rais akiwa katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (wa pili kulia)wakati wa mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Pertamina ya Jakarta Nchini Indonesia,(hawapo pichani ) katika Ukumbi wa Ofisi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN) Mjini Jakarta Indonesia ,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Pertamina ya Jakarta Nchini Indonesia,unaoongozwa na Kiongozi Daniel S.Purba (wa pili kulia) mazungumzo hayo yalifanyika jana katika ukumbi wa Ofisi ya Jumuiya ya Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN) Mjini Jakarta Indonesia ,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla. Picha na Ikulu. 

Post a Comment

0 Comments