MAZISHI ya mama wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, marehemu Asteria Kapela, yamefanyika jana Agosti 1, 2018 katika kijiji cha Bupandwamhela Wilayani Sengerema yakihudhuriwa na maelfu ya wakazi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza.
Katika usia wake, Shigongo amesema kuwa hakika ni pigo kwake na kwa familia kwa ujumla kwani ameondokewa na mtu muhimu katika maisha yake na Mwenyezi Mungu ampumzishe katika nyumba yake ya milele daima kwani atamkumbuka siku zote za maisha yake na ataendelea kutenda yale yote aliyojifunza kutoka kwake.
Paroko wa Kanisa Katoliki Mwangika Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu, Padri Hilary Faraja, akiongoza ibada fupi ya kumuombea marehemu.[/caption] Katika mazishi hayo viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wamejitokeza kuungana na familia hiyo katika msiba huo, ambao ni pamoja na Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Buchosa (CCM) Dkt. Charles Tizeba, mbunge wa zamani wa Nyamagana na aliyekuwa waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Lawrence Marsha. Pia miongoni mwao ni Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nauye, na mchekeshaji Masanja 'Mkandamizaji'.Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo (wa kwanza kulia) akiwaongoza ndugu zake kuweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu.Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (wa pili kushoto), Mhasibu Mkuu wa Global Group, Laurence Kabende , akifuatiwa na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally, wakiwaongoza wafanyakazi wa Global Group kuweka shada la maua kwenye kaburi.Watoto wa kike wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi.Dada wa marehemu wakiweka shada la maua.Hawa ni ndugu wa familia. Wajukuu wa kike wa marehemuDkt. Charles Tezeba akiweka shada la maua.Baadhi ya wajukuu wa kiume wa marehemu.[/caption] [caption id="attachment_231650" align="alignnone" width="1024"]Laurence Masha.Paroko wa Kanisa Katolikia Mwangika Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu, Padri Hilary Faraja.
0 Comments