DOGO JANJA ANA HADHI YA KUWA MUME WA MHESHIMIWA

DOGO JANJA ANA HADHI YA KUWA MUME WA MHESHIMIWA



Staa kutokea kwenye Bongo Movie Irene Uwoya amefunguka kuhusiana na uteuzi wa Jokate Mwegelo kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, baada ya kupewa ushauri na mmoja kati ya wasanii wenzake ambaye ni Rado katika ukurasa wa instagram.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Rado ametuma ujumbe mrefu wenye kuhoji na kumshauri Irene Uwoya nafasi yake katika siasa alichokifanya kipindi cha kampeni ya Urais mwaka 2015 na hivyo Irene Uwoya alionekana kuupata ujumbe huo na kumjibu Rado kupitia ukurasa wake wa instagram.

“Habari ya asubuhi ni nzuri kwangu na asante sana kwa ujumbe,Naamini sana na kuelewa katika mtazamo wako uliopendekeza na kutamani kutoa majibu chanya,Rado kaka yangu napenda kusema haya”>>> Irene Uwoya

“NAAMINI SANA SANA KATIKA MAAMUZI NA MAPENDEKEZO YA MWENYEKITI WANGU WA CHAMA.Naamini sana na nimependa sana katika uteuzi wa Jokate sababu baada ya kampeni na uchaguzi kuisha watu weng tuliendelea na mambo yetu binafsi lakini ukifuatilia kwa umakini”>>> Irene Uwoya

“Jokate amepambana na amekuwa karibu sana na harakati za chama na haswa kushiriki katika shughuli za kijamii kwa haya na mengi zaidi mimi nampongeza na kiukweli alipanda mbegu nzuri ambayo amevuna mavuno mazuri sana na hongera sana kwa Mheshiwa Jokate Mwegelo.Na pia amini katika hili wakati wa MUNGU ni wakati sahihi zaidi na still bado tuna muda na matumaini pia.Nitafanyia kazi pale nilipokosea na kurekebisha Asante”

Post a Comment

0 Comments