BILLNAS AMSHAURI STEVE NYERERE AFUNGUE BIASHARA YA MAMBO YA MISIBA

BILLNAS AMSHAURI STEVE NYERERE AFUNGUE BIASHARA YA MAMBO YA MISIBA




Msanii wa Bongo fleva anayetamba na kibao chake cha Labda Bill Nas amempa ushauri wa bure msanii wa Bongo movie Steve Nyerere na kumtaka afungue kampuni yake ya binafsi itakayoshughulikia mambo ya misiba.

Steve Nyerere siku za hivi karibuni amekumbwa na skendo ya Kula fedha za rambi rambi zinazochangwa na watu kwa ajili ya kuwafikia wafiwa.

Steve Nyerere na Billnas waliingia Kwenye bifu zito mapema mwezi huu baada ya Steve kumwambia maneno kuhusu yeye na Nandy jambo ambalo halikumfurahisha kabisa Billnas.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Billnas ameibuka kumtaka Steve kuweka ugizaji wake wa vichekesho pembeni na badala yake ajikite kwenye biashara ya kuandaa misiba maana ndio anayoiweza:

Steve badala ya kutumia pesa zake kuandaa comedy shoo kubwa sijui anaweza kufungua kampuni ya kushughulikia mambo ya misiba na inaweza kuwa kampuni kubwa tu na akatengeneza hela na akatumia mtaji huo huo mdogo akanunua magari ya kubebea maiti na akafanikiwa zaidi”.

Post a Comment

0 Comments